Ushauri!!

Updated on May 23, 2017 in ShostiTalk
3 on May 5, 2017

Jamani wapendwa wazima? Wakubwa shikamooni…
Naombeni mnisaidie mwali wenu nipo njia panda, wakati nakaribia kuolewa kuna X wa mume wangu alikuwa msumbufu kutwa kupiga simu nikamuuliza muhusika akasema sababu ameamua kuachana nae ndo maana anamsumbua. Basi mimi nikaelewa ila nikamuomba amkanye.
Miezi minne baada ya ndoa nakuja kuona kipimo cha ujauzito wa huyo X kwenye suruali ya mume wangu nikamuuliza mume wangu akasema ndivyo anavyodai kuwa ana ujauzito wake kiukweli niliumia sana, nikamùuliza mwenzangu kwanini umenificha siku zote akasema sababu huyo mwanamke alishaachana nae na hakumwambia kama mjamzito kaja kumwambia anaujauzito baada ya miezi miwili hivyo kamwambia wasubiri mtoto azaliwe. Nikamuelewa ila kipindi chote alikuwa msumbufu kudai pesa za kujikimu sijui za clinic, Mungu kamsaidia akajifungua salama sasa hivi mtoto ana mwaka hataki kufanya vipimo anasema anataka huduma. Ushauri wangu je endapo atakubali kufanya vipimo ikiwa positive nilipokeaje ? Sitaki kujihusisha kwa lolote lile juu ya huyo mtoto. Sijajaaliwa mtoto bado ila naamini nami nitajaaliwa muda atakaonipangia mwenyezi

  • Liked by
Reply
1 on May 19, 2017

my dear pole sana maana umeingia tu na kukutana na mizigo ila usihofu mumeo anakupenda ndio maana akamuacha Huyo na kukuoa we. mtoto hana kosa so ikitokea positive mpe ushirikiano mumeo na mpange matumizi mtakayokuwa mnatuma kwa mwezi. hakikisha haugombani na mumeo juu ya hilo maana utampa nafasi ya kurudi kule kutafuta faraja

on May 23, 2017

Kweli kabisa mama ushauri umesema sawa ingawa roho inauma, maana mwanzo wa kuwasiliana kila wakati ndio mwanzo wa kurudiana na hakuna kitu chenye nguvu kama mtoto…ila kuwa makini na huyu bidada na mumeo

Show more replies
  • Liked by
Reply
Cancel
0 on May 23, 2017

Maadam aliamua kuwa na wewe basi ujue alifanya maamuzi yake sahihi na kwa nini hakutaka kuwa na yule. Ila kama yasemekana mtoto ni wake basi make sure mtoto anapata huduma. Na isiwe issue ya masimango kwa mumeo juu ya mtoto. Tulia na mumeo usiwaze ya nje wewe enjoy the moment

  • Liked by
Reply
Cancel
Loading more replies