Topic kutoka kwa blog :: NIPO KATIKA MAHUSIANO LAKINI SIWEZI KUACHA NDOA

Updated on January 10, 2017 in ShostiTalk
11 on April 22, 2016

Nahitaji mtu anisaidie kurudisha maisha yangu katika mstari ulionyooka, nirudi kuwa mama na mke niliyekuwa mwaka uliopita, kitu cha muhimu zaidi kwangu ni familia yangu, ndiyo iliyokuwa inanipa ujasiri bila kutegemea kurudishiwa kitu chochote. Mapenzi hayana gharama na kama mama, ni kazi yangi kuwapenda, kuwalinda na kuwajali. Sikuwa nategemea vitu vingi kutoka kwa mume wangu na yeye hakutegemea vitu vingi kutoka kwangu. Tulikuwa ndoa nzuri, hatukugombana sana, tulikuwa na furaha pamoja na watoto wetu.

Yote yalianza pale ambapo baba wa mmoja wa watoto pale shuleni (hana mke) alikiri kwangu kuwa namvutia na kuwa alikuwa ananitamani kwa muda sana. Ilinishangaza sana! sikutegemea kuwa mmama kama mimi ningeweza kuwavutia wanaume wengine zaidi ya mume wangu.

Nilimkatalia, lakini kuanzia kipindi hiko ujasiri wangu ukaongezeka na nikaanza kufurahia hilisuala kwamba kumbe wanaume wengine bado wananitamani

Miezi sita iliyopita, nilikutana na William(siyo jina la kweli). Alinivutia sana, kimwili na kimapenzi. Tulianza kutumiana sms, mwanzo ilikuwa kawaida tu, tuna flirt. Tulikutana mara kwa mara tukienda kunywa pamoja na kuenjoy, tukifurahi na kucheka. Urafiki wetu ukazidi kukua na kukua.

Mi sio mtu wa kudate date ovyo wala kutoka ovyo, lakini ghafla nikajikuta nipo katika mahusiano na huyo William. Yale mahusiano haswa, mambo motomoto. Kipindi nilipojishangaa na kujiuliza nafanya nini, ilikuwa nimeshachelewa, nilikuwa nimeshalala nae. Najua ilikuwa kosa kubwa sana, najua nimefanya kitu kibaya sana na mume wangu kamwe hatonisamehe akijakujua kilichotokea.

Nikajiuliza, ninataka nini katika haya mahusiano na William? Je, nipo naye kwa ajili ya kufanya naye mapenzi tu? Kimwili wote tunapendezana, wote tunatamaniana, lakini William aliniambia mahusiano yetu sio kwa ajili ya kufanya mapenzi tu. Aliniambia kuwa ananijali na anataka awe ananiona kila weekend. Akaendelea kuniambia kuwa anani miss kila nikiwa mbali naye, akawa ananitumia sms ambazo zinanikosha haswa.

Nilianza kufikiria kuwa nimeanza kumpenda William maana masaa 24 alikuwa akilini mwangu, nilipenda sana kuwa nae, kuspend nae muda, kucheka nae. Nilivutiwa nae sana kiasi cha kwamba nilikuwa sivutiwi na mwanaume mwingine yeyote.

Tatizo likaja hapa, siwezi kuondoka na kuacha ndoa yangu, siwezi kuiacha familia yangu, mume wangu, watoto wangu. Sitaki kabisa kuiharibu familia yangu. Nilichonacho ni kitu kizuri kuliko kitu chochote duniani na siwezi kukiharibu kwasababu ya makosa yangu niliyofanya, lakini siwezi kuacha kuwasiliana na William hata nijaribu vipi, kila mara huwa naishia kurudi kwake tena na tena! Nimekuwa kama mtu ambaye hawezi kuacha madawa na William ndio hayo madawa.

Hata kama Williama ameniambia kuwa ananipenda, hajafanya kitu kunihakikishia kuwa haya mahusiano tuliyokuwa naye yana future yoyote. Huwa najifikiria mwenyewe nikiwa nae bila watoto wangu, hiki kinaniumiza sana.

William hana mtu, yeye yupo single, na sidhani kama ataweza kubadilisha gari lake la ki-bachelor convertible lenye siti 2 tu na kununua gari la familia. Kila kitu katika maisha yake kipo ki-bachelor. Hata sehemu anayoishi siyo mazingira ya watoto kuishi kabisa, siwezi ata kufikiria watoto wangu wakiishi mule na kikubwa zaidi ziwezi kufikiria kuwa William atakubali kubadilisha sehemu yake ya ki-bachelor na kupata sehemu itakayo wafaa watoto wangu.

Ishara zote zinaniambia kuwa mimi ni msichana wake wa kumpitishia muda tu, na akipata msichana mzuri aliyekuwa single ataniacha na kutulia naye huyo. Kuna muda nimewahi kuanzisha mada hii na yeye kwa njia ya utani tu, na akakataa. Laziama akatae, hataki kujiharibia. Na sina mamlaka ya kumlazimisha wakati mimi mwenyewe ni mke wa mtu. Aliwahi kuniambia kuwa itanibidi niamue kama nataka kuwa naye kikweli. Inamaanisha naona wivu kunishare na mwanaume mwingine? sielewi

Hakuna kushare tena, mimi na mme wangu tumekuwa kama watu tusiojuana sasa, hatuna connection kabisa, mme wangu hanivutii kabisa kama ilivyokuwa zamani, hata nijaribua vipi. Nadhani ni kwasababu William ananichanganya, Najua haya mahusiano yatakuja kunilipukia tu, mme wangu atakuja kugundua mambo niliyokua nikiyafanya.

Katika ndoto huwa najiona nikiondoka na kumuacha mme wangu na kuenda kuishi na William, kuanza maisha mapya na William, lakini siwezi kumuacha mme wangu na inaniuma kumuacha mme wangu, itamuua nikimuacha tu.

Na huwa nafikiria kama William anathamani kubwa kiasi gani hadi mimi niwaumize watu wenye thamani kubwa kuliko kitu chochote kwangu duniani.Nikiacha ndoa yangu kwa ajili ya mtu mwenye thamani kubwa, ya kila chozi na kila maumivu ili kuwa na mahusiano mazuri na yenye furaha zaidi. Hiyo ingekuwa vizuri sana lakini sidhani kuwa William ni huyo mtu.

Je nimkazie William na kumlazimisha aniambia ukweli? Ukweli wa kitu gani anachokitaka kwelikutoka kwangu. Anatkiwa anipe uhakika fulani kuwa ata-commit kwangu. Nafikiria kuwa William hawezi kuwa katika mahusiano ya kutulia, na nikiangalia nina watoto. Lakini kumuuliza yote haya inaweza kufanya nikamkosa William, anaweza kuniacha na raha niliyokuwa nikiipata nisiipate tena.

Na je, akikubali kuwa ataweza ku-commit kwangu pamoja na watoto wangu, nina huo moyo wa kumuacha mme wangu, kuiharibu ndoa yangu na kuwaharibia furaha watoto wangu?

Naombeni mnisaidie, kama kuna mtu yoyote amewahi kupitia jambo kama hili. PLEASE! naomba mtu aniamshe.

Hii ni story ya kweli kutoka kwa mdada anayepitia mambo haya

 • Liked by
Reply
1 on April 22, 2016

Subiri kutumbuliwa jibu na mumeo

on April 23, 2016

Mhhh, nadhani familia yako ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote.  Please please please baki na Mumeo na wanao.

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
0 on April 25, 2016

Mamaaa weee….Unabalaa haswa, embu anza taratibu kumuacha huyo willy kama unahitaji familia yako, maana mwisho wa yote utakosa vyote. Ni hatari mno

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on April 25, 2016

i advise you ku accept the fact kua umeshaolewa na ulipenda once na kumkabidhi moyo wako mwanaume mmoja tu na mkatengeneza familia…wanaume hawana gurantee so william can change anytime at the moment umeshamuacha mume wako,ukajikuta unakosa vyote na kubaki unahangaika..hiyo ni feeling ya mpito tu,unaweza ukatengeneza mazingira na hizo raha ukazipata kutoka kwa mumeo km zamani…mume au mke wa kwanza ni wa kwanza tu,think about the kids and the union btn you and your husband,
please please u may kuchepuka na kunogewa in marriage but never forget abt the family you built with all the love.

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on April 25, 2016

mwe huyu mimi sioni kama anahitaji ushauri. majibu yote anayo. yaani ukiisoma hiyo story anajijibu mwenyewe. kwamba anajua hana future na william na hawezi kuwaacha watoto wake na anajua william hawezi kubadilisha maisha yake ku accomodate hao watoto.
naona cha kwanza ni kutubu kwa Mungu wake amsamehe. na kutubu maana yake kuacha kabisa mawasiliano na huyo willey. atafute vacation aende na mumewe mapenzi yatarudi.

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on April 27, 2016

Du…..!!!!! Is this serious? She can’t be serious….!!!Mmhh…haya majaribu yatupite mbali. mama Ushauri umeongea vizuri., kama yuko serious afate ushauri wako. Ila pia wamama tutulie jamani, hata kama tunaumizwa.

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on May 3, 2016

Mh me nilidhani story ya kuigiza!!!!ngoja nijaribu kumshauri cha kwanza kubali umekosa tena uliyemkosea wa kwanza ni Mungu then mumeo halaf watoto.Km kweli unaithamini familia yako achana kabisa na huyo Willy yaweza kuwa ngumu sababu ya hisia ulizoziweka kwake ila anza kwa kutubu kwa Mungu then kuwa karibu sana na Mungu km mkisto nenda kanisani mara kwa mara na kama muislam jitahidi kufanya sala.Kwa kufanya hivyo utamuondoa huyo Willy kwenye mawazo yako.Sasa baada ya hapo anza kufanya majukumu yako km mama na mke kwa bidii yaan kuwa na muda mwingi na watoto wako pia na mume.Hope inaweza saidia.Ila ndugu yangu wewe mumeo akijua HUNA NDOA HAPO.

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on May 3, 2016

mbona kashasema hawez acha familia yake..huko kwa william anafuata nini?
hzo tamaa za kizamani khaaa…rudi kwa mumeo tengeneza futureyako na watt wako
achana na william..

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on May 3, 2016

mweeeeh pole…hapo taratibu anza kua nae mbali ikibid safiri hata kwa muda nenda kwenu labda huko utatafakari zaidi..ila kama bado utakua unamuona kila siku aisee hapo itakua ngumu na ukichoka sasa FUMANIWA YAISHE…japo sipendelei hili shoga watu tunatafuta  ndoa hata za kamba ukikaa na huyo william utamzoea atakuzoea then atapata cha nje tena alafu ukose yote.

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on May 5, 2016

jaman kama mumeo hana shida yoyote usifanye hayo ni mapito tu! achana na willy angalia maisha yako tu na familia

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on January 10, 2017

kazi MBAYA  ukiwa nayo, ukiwa huna NZURI. sasa we mwendekeze Will mumeo akikuacha na wewe Chali, ” MUNGU HAPIGI KWA FIMBO HUPIGA KWA ZAKE NJIA” (SABAHA SALUM mCHACHO)

 • Liked by
Reply
Cancel
Loading more replies