MUME WA MTU

Updated on November 19, 2015 in Mapenzi na Mapendo
51 on November 6, 2015

me swali langu haliiitaji hata kutaja umri…..hivi mtu anaposema ”Nina nyota ya KUPENDWA NA WANAUME ZA WATU” hua ana maana gani?maaana nakua sielewi anakua usoni ana chata flani?ama n vipi?mwingine anasema hivyo kwa furaha na mwingine atasema hivyo kwa huzuni….

 • Liked by
Reply
2 on November 6, 2015

ninacholelewa hapo ni kama kismati cha kupendwa na aina fulani ya watu,mwingine atakua anafurahia kwa sababu anapendezwa na hio hali na mwingine hafurahi maana hapendezwi nayo,mfano unakuta mschana yuko katika kutafuta mtu muafaka wa kupanga nae maisha na kuoana sasa hapati huyo mtu anapata waume za watu tu hapo hawezi kufurahi na mwingine unakuta ni mschana wa mjini tu shida yake pesa sasa hao waume za watu yeye ndio mwakeee hapo waje hata mia yeye ndio anafurahiii yeye ni pesa tu

on November 7, 2015

kweli inakera sana,pale unapomuomba mungu kila siku akupatie wa kwako mwanaume ambae yupo single lakini unaishia kutongozwa na kupendwa tena na kudekezwa juu na mume wa mtu,na hizi haja za mwili na sie wanawake tukidekezwa na kulelewa kama yai na mwanaume tunajikuta automatical unajiachia nae ukizinduka unakasirika unamtimua akija kukubembeleza unamrudia huku ukijisemea ngoja tuu niwe nae kwa mda mpk pale nitakapopata ambae hajaoa maana lasivyo utaishia kugawa papuchu kama pipi kwa vijana ukidhani utatulia nae kumbe mwenzio anataka kukupitia,jamani sio siri kwa upande wangu nashukia sana na nina hiyo nyota kila anayenitongoza na kutaka kusettle na mie ni mume wa mtu,yaan nina chukia na sina jinsi labda ipo siku mungu ataniona na kuniondolea hii nyota.

on November 11, 2015

Hiyo mdogo wangu sio nyota hilo ni pepo tena inabidi ulikemee kwa nguvu zako zote.

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
4 on November 6, 2015

yaani mimi naamini kuna matukio yanakuwa yanamtokea mtu kutokana na background yake.

1: Family curse/blessings
kuna laana au baraka zinazotembea ktk familia au ukoo ndio pale utasikia wale kwao wote wamezaa na waume za watu, au wale kwa waume za watu hatari.so hiyo mtu inakua sio choice yake bali ni nature inalazimisha.

2: Maneno uliyowahi kujienea huko nyuma hasa wakati unakua.
Yes maneno yanaumba. mfano kuna watu wakiwa wanakua wanaona mfano wa dada zao, ma aunt na majirani wakipewa maisha na waume za watu. binti anaanza kuota na kukiri kwamba akikua atapenda apate mume wa mtu amhudumie. ndivyo inavyotokea. kuna kitu kinaitwa the law of attraction. yaani what you think about you bring about. ukiangalia maisha yako ya sasa utaona ni vitu ulivyokua unaviota zamani

3: laana ya kujitakia
sijajua ukweli wa hili bali inasemekana ukionja tu mume wa mtu basi nyota yako inakuwa ya waume za watu. watakufuata hao tu hutapata kijana mwenzio.pia mwenye mume akigundua uko na mume wake na akakutamkia laana ni rahisi kukupata. so akikunenea kuwa utaishia kuwa kimada ndivyo itakavyokuwa.

4: jini mahaba
hili huwa halipendi msichana aolewe. hivyo litakuwa linakuletea waume za watu ili usiolewe.

5: the way you carry yourself
yes kuna jinsi unajiweka una attract waume za watu tu na sio masingle man. jiweke ki wife material na si kishangingi! mwe nimechoka kuandika ntaendlea baadae

on November 6, 2015

Mhh mama ushauri umegusa engo zote, lakini pia hakuna cha nyota wala nini ni tamaa tu ya wasichana wengi wa mjini wanaopenda short cut ya maisha sasa atajustify vipi upuuzi anaoufanya, ndio hivyo anajitia ana nyota ya kupendwa na waume za watu.

on November 7, 2015

lulu hapo napigana na wewe,sio wasichana wote wanaofatwa na waume za watu wanatamaa ya pesa hapana,binafsi siipendii hii hali na wala sina tamaa maana nina uwezo unaonitosheleza kabisa ila nachokosa ni mapenzi na kujalia na binadamu wa jinsia tofauti na mie kwa bahati mbaya wanaokuwa serious namie na wanaodumu kwa muda mrefu ni wanaume za watu na kwa bahati mbaya sijui nzuri mie sinaga tabia ya umalaya au kuhangaika na mwanaume zaidi ya mmoja,je mtu kama mie utaniweka kundi gani?na hata hao wanaume wananishangaaga kwanini siolewi wakati nina sifa zote za kuwa mke naishia kuwajibu mimi mwenyewe sijui labda muda wa mungu kuamua bado,ila sasa mama ushauri umenifungua kitu kutokana na ushauri wako lazima kuna kati ya hayo mambo uliyosema yananisababishia.kuanzia leo nitakazana na kufunga kwa maombi ili namii niwe huruu na hili janga.

Verified
on November 7, 2015

Mama Ushauri umeongea vizuri sana …. na mimi nimepatamo funzo humo

on November 11, 2015

Ni kweli Queen sio wote but majority huwa ni wale wanaopenda pesa kwani wenyewe wanadai wanaume za watu wanajua kuhonga. Ushauri wangu kwako- kama uko na mume wa mtu ni bora uachane nae muombe Mungu atakupa wako ukiwa na mwanaume inakuwa ni vigumu kumpata mwanaume mwingine kwakuwa hata aliye single ataogopa kukufuata akijua wewe una mtu wako tayari.

Show more replies
 • Liked by
 • 1
Reply
Cancel
1 on November 6, 2015

yaaani mama ushauri wala hujanichosha….nimekuelewa vizuri mnoooo…

on November 11, 2015

Nagy na wewe unahiyo nyota?

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
1 on November 7, 2015

na mume wa mtu anayependa kutembea na wake za watu huwa anatafuta nini hasa?

on November 11, 2015

Huyo anaogopa majukumu anajua mke wa mtu anahudumiwa na mume wake yeye kazi yake ni kitandani tu hana jukumu lingine.

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
3 on November 7, 2015

Yes Queen kama una nia ya dhati ya kuolewa hebu muache huyo mume wa mtu kabisa. kaa mbali nae. jaribu kuwa single kwa muda huku ukimuomba Mungu akupatie wa kwako. utampata tu kwani una dhambi gani mpaka Mungu asikupe? kumbuka wengi wetu tumepita huko kwa hiyo hatuwezi kukuhukumu

on November 7, 2015

hatua ya kwanza ni kumuacha huyo jamaa. usitegemee kumpata wako wakati uko na wa mwingine. utakuwa unamconfuse Mungu asijue nini unachokitaka

on November 11, 2015

Ni kweli kabisa mama ushauri, hata kama kuna kijana anakufuatiria akikuona na mwanaume mwingine unamtia uoga anajua kuwa umeshampata umtake. Unaweza ukawa unajizibia rizki ya kumpata wako wa ubani bila mwenyewe kujua. Ila jamani twende mbele turudi nyuma waume wa watu wanajua kumteka mtu yaani mpaka ukija kuzinduka muda ushaenda umeshamzoe kwenye kuachana ndio kasheshe.

on November 12, 2015

yaaaan dada angu lulu upo sahihi kabisaaaa,jamaniiiii mie najutaaa na machozi juu,nitamuachajee huyu mwanaume nimekuwa nae mwaka na nusu sasa, ananijali utasema hajaoa na kwenye ndoa yake wanaamani tele najua kutokana anavyoongeaga na mkewe kwenye simu na sms zao wanazotumiana,.mwanaume anajua kupanga mambo yake mpk namshangaa ni mhaya ana miaka 37 mie 26,hapa nawaza mambo ya kurudi kuwa single na lonely mpk ntakapompata huyu ambae hajaoa nitaweza kweli na nilivyomzoea huyu jamanii kwa ushauri wake,anavyonijali,anavyonisaidia kwa mambo mengi,nitaweza jamanii kumuacha tuu bila ugomvi,naomba mnishauri unamuachaje mtu bila kuwa na ugomvi,maana kusema ukweli nikimpa sababu ya mie kutafuta mtu single alishasema wewe siku ukipata mtu anataka kukuoa na yupo serious niambie tuu nitaku let go, ila kamwe sitaacha kukupenda maana anasema tangu awe na mimi amekuwa na furaha sana hadi kwenye ndoa yake furaha na amani imerudi na naamini ivyo maana nimeona

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
5 on November 7, 2015

Mmmh queen mwenzangu na mm ni km wewe. Tokea nimeachika niko in relation na mume wa mtu mwaka wa tano sasa na wala siko nae kwa ajili ya pesa. Mm nina uwezo Wangu alhamdulillah. Siko nae kwa matumain ya kuolewa nae lkn sipat mume ambae yuko single. Wote in double ūüėāūüėā. Watu wakiniuliza una mume nikiwajibu no wananiambia mm nachagua. Kazi kweli.

on November 9, 2015

kwa nini msioane tu Ashqueen mkawa dhahiri,miaka mitano si michache

on November 10, 2015

Wallah nahic km m not ready kuingilia ndoa ya mtu. While in real sense i do ingilia but i dont want it to b official. Napenda niwe na mume wa pekee yng. Amyluv

on November 11, 2015

endelea kuomba Allah atakujalia hitaji la moyo wako..Inshallah

on November 11, 2015

Wanawake tumekuwa wengi kuliko wanaume kama sheria ya dini inaruhusu ni bora basi muoane kuliko hivyo mlivyo. Pia kwakuwa bado uko na huyo hata huyo wa peke yako unamkimbiza kwakuwa anajua kuna mwenzake. Inshaalah Mungu atakuletea wa peke yako ila muombe akupe ujasiri wa kumuacha huyo kwanza.

on November 11, 2015

Asante kwa ushauri na kuniombea nipate wa pekee. Ntajitahid kufuata ushauri wenu

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
0 on November 9, 2015

mama ushauri umetisha sana kwa kweliii

 • Liked by
Reply
Cancel
3 on November 10, 2015

mama ushauri umemaliza yotee aiseee….wengi hawaelewi haya mambo ni kiroho na vile unatenda ipo siku utatendewa tu kama sio kwako ni kwa watoto wako….mi nliachaga hayo mambo zamaani baada ya kukutana na watu wakanielezea na madhara yake kabisaaa na kweli nikaanza kuyaonaa…Namuomba Mungu anipe wa kwangu bado namngoja na naamini atanipaa ila waume za watu nyota yake inipitie mbali kabisaa sitaki yale machozi ya wake zao ni kujitafutia laana zisizo na msingi

on November 10, 2015

Mungu atakupa Kamwali mradi umeshaamua kuachana nao utapata wako

on November 10, 2015

Mhhhhhh!! Mama Ushauri kaongea kweli.  Ambao mpo single na mnaandamwa na waume za watu ni vema kusali na kumlilia Mungu.  Na sala/dua njema ifanye saa tisa usiku pakiwa pametulia na uwe umedhamiria hasa, Mungu hamnyimi aombae kwa dhamira. Mlilie Mungu kimaombi.

on November 11, 2015

Ameen Kamwali, kila mwenye kusubiri yuko pamoja na Mwenyezi Mungu.

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
5 on November 10, 2015

kukaa single huenda kunaumiza single ladies ila mara elfu 5 kuliko mume wa mtu..jamani mi niliwahi kumdate mmoja kabla sijaolewa huyo kaka mwanzoni sikumpenda ila nilishawishika alikuwa ananijali mno huku nimetoka kupigwa kibuti kitakatifu…naposema kitakatifu uwiiiii acheni Mungu aitwe Mungu..jamani siku nimemkubali huyo kaka aiseee alijua kunipa pepo..nilikuwa 3rd year na chuo nilirudia mwaka..nilikuwa nakula bata kuku hawanifai…sasa after few month jamani nilimpenda huyo kaka kama sijawahi kupenda siku za nyuma.mkewe akaja akajua nahisi alinipa laana…uwiii huyo kaka¬† alikuwa na cash na alijali sana familia yake kwa pesa tu..hakuwa na muda nao kitu ambacho naomba Mungu kisinitokee..sasa mkewe naona alikuwa ananililia kwa Mungu wake asubuh mchana na usiku..yakanifika from no where mume mapenzi yakarudi kwa mkewe mie napewa hela tu …..aiseeee kilikuwa kibuti cha kizungu¬† sana sana lakini hakivumiliki..ila sina jinsi mkaka ndio karudi kwa mkewe na hela aliyokuwa ananipa nilikuwa nakulia bata mara nairob,arusha ,dar, mwz..yani ikifika weekend kama nawashwa au nakazi….basi alivyoniacha nikakaa gud 3 years sipati mtu permanent wote wazinguaji..nikampata mmoja nikakaa nae atleast nikapata mimba nilipomwambia akaniacha…Mungu ni mwema sikutoaga hiyo mimba nao namtoto mzuri sana sana na nimeolewa na mtu anaempenda sana mtoto na mm…

moral of the story..wasichana machozi ya wanawake mabaya,mume anauma sijui nisemeje  na hakuna siri..usijisifie na nyota au nimekaa nae miaka kadhaa..please achana nae kwanza ..invest kwa Mungu mwambie shida yako na nn unataka atakupa wako kwa jinsi utakavyo..unajipotezea muda na unajipotezea mahusiano yako na Mungu amabae mtoa mume..ni kweli kuna wakati wa Mungu utapata .my friend sugua goti ufike utashangaa unafika ukiwa 40..sijui utaenjoy nn.

sorry kwa gazeti…achaneni na waume za watu, hawana faida ni hasara sana mbele yako

on November 10, 2015

nimelipenda somo lako…..ubarikiwe

on November 11, 2015

Hongera na pia pole kwa yaliyokufika @Heleen, story yako inagusa

on November 11, 2015

mimi hua nafikiria mbali sana wanawake wengine washirikina anaweza kuendea kwa babu ukajikuta unableed mwaka mzima,,,hahaaa

on November 11, 2015

Asante Helen umeongea yote. Mbaya zaidi kuna wanawake wengine akishakuchukulia mume wako atafanya kila njia ujue kuwa anatembea na mumeo, matusi yatakuwa yako akiwa na bwana ukipiga cm yeye ndio wa kwanza kupokea. Mke mtu atalishwa mbilimbi na ukwaju mwitu kisa mumewe unaye wewe kwakweli huyu manamke akimlilia Mungu wake lazima yakupate ya kukupata.

on November 12, 2015

amyluv kweli, mwingine akijua uko na mumewe anakutia uchizi au anakufunga uwe tasa kabisa. unashangaa ukiolewa hupati mimba wakati huko nyuma ulishawahi kuchoropoa. na wengine wanakuua kabisa. kwa hiyo kuna madhara yake hasa huku afrika kwenye mauchawi. ila wanawake wengine pia wanawaendea kwa waganga hao waume za watu basi familia inasahaulika mazima. naionaga sana kwenye movie za kinigeria. mbaya sana hii kwa kweli. tuombeage na hizi ndoa jamani Mungu azitetee

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
6 on November 10, 2015

Heleen somo zuri sana. kuna mahali nilisoma kitu kinaitwa 8020 rule. pia inapatikana kwenye movie ya why did i get married (tunajifunza kutokana na movies pia). hii 8020 rule inasema kwamba, katika kila relationship, satisfaction ambayo iko guaranteed ni 80% only. yaani yule partner wako hawezi kuwa exactly vile unavyomtaka ambayo ni 100% bali akijitahidi sana ataishia kwenye 80%. ina maana ile 20% tunavumiliana. yeye anakuvumilia wewe na wewe unamvumilia yeye. sasa wanaume (au wanawake) wanaotoka nje huwa wanaenda kutafuta the missing 20%. baada ya muda anagundua kwamba ameacha 80% kwa ajili ya 20% ndio unaona anarudi kwa mkewe. mara nyingi mahusiano haya huishia kwa jamaa kurudi kwa mkewe afu mdada unabaki kujiona umetumiwa tu which is very bad.

on November 11, 2015

mama ushauri…sure usemalo.yani wanaodate waume za watu huwa wana assumption ifuatayo..KWAMBA IPO SIKU JAMAA ATAMUACHA MKEWE.my friend ur wrong.ndoa¬† ni mpango wa Mungu .chance iliyopo ni probability.yani yaweza isitokee au hata ikitokea ipo mbali sana uvumilie hasa.anamuacha mkewe akuoe ww..

ngoja niwape somo dogo…yani ukijiona na ww fresh unaolewa na mume alishawahi kuoa ujue ww ndio ujipange….yani ww ndio beginer yeye yuko far ahead anajua ujinga na upumbavu wote wa ndoa..inamaana ujitolee kuumia …yeye kila alifanyalo ni marudio wakati ww unaanza..Jamani ndoa ni tamu ila wate muwe wanafunzi fresh sio yeye aoe ndoa imshinde ww useme utamuweza ….yawezekana kweli utamuweza¬† ila tunaziita probability.kuna chance tu na sio 100 percent

on November 11, 2015

Hapo kwenye kuwezana ndio panakuwa na utata na ndio maana utakuta wanawake wengi walioolewa baada ya kuwatoa wenzao ndani wanaishiaga kuumizwa tu. Mbaya zaidi hata kuondoka unashindwa kwa jinsi ulivyoingia kwa matashtiti. Jamani wanaume viumbe wazito yaani kuishi nao kwakweli ni kuvumilia tu.

Lakini pia kuna wanawake wengine jamani hata hiyo 80% hafiki anakuwa 50% sasa mwanaume akienda nje kutafuta missing 30% anakutana na full 80% hapo bi shosti mwanaume anakuhama na harudi tena. Cha muhimu ili kupunguza mahangaiko ya ndoa kina mama tujitahidi angalau kuifikia hiyo 80% hata akienda huko akumbuke kurudi.

on November 12, 2015

Lulu nakubaliana na wewe. mimi kabla sijaolewa nilikutana na jamaa alikuwa mume wa mtu lakini pia alikuwa bosi wangu. huyo jamaa tukawa tunatoka nae lakini hakuwahi kuniomba tufanye mapenzi. yaani nilikuwa na mshangaa sana. lakini alikuwa ananisimulia vituko anavyofanya mkewe mpaka nikawa namuonea huruma. mke ni mbabe kama dume, ananuna miezi hata sita haongei na mtu including watoto. ikabidi watoto wapelekwe kwa bibi hapa hapa dar. huyo jamaa ndo anapika ndo usafi ndo kila kitu. so lengo la yule jamaa halikuwa kucheat bali alikuwa anafuta companion. mtu wa kumueleza shida zake na kukaa tu kurelax kujisahaulisha machungu ya nyumbani. huyo mke nadhani atakuwa kwenye 10% so jamaa anatoka kutafuta 90%! ukiacha tamaa za wanaume hata sisi tunachangia sana wenzetu kucheat!

on November 13, 2015

mama ushauri wanaume wengine waongo pia anatumia kusema madhaifu ya mkewe ili apate anachotaka kumbe hamna lolote,anakuelezea ooh mke wangu hivi na wewe unaingia huruma unampa papuchi siku mbili tatu huyo kwa mkewe na sie wanawake tulivyo mwalimu wetu kipofu ukisikia hivyo ndio unajitutumua ili asahau kule na kwa mganga unaenda dawa zikiisha anarudi kwa mkewe cha muhimu ni kumomba mungu tu upate wako la sivyo mume wa mtu siku zote ni wa kupoteza muda tu..

on November 13, 2015

ammy ntakupeleka kwa urojo wa husna kariakoo…..

on November 17, 2015

haya Nagy nasubiria

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
1 on November 11, 2015

mama ushauri kula urojo kwa selebonge jioni nakuja KULIPA AISEEEEE…hiyo 8020 rule aiseee ni ukweli usiopingikaaaa kabisaa…nimeelewa somo sanaaa haswa kwa heleen kweli

on November 12, 2015

hahaha kamwali hujatulia

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
2 on November 12, 2015

Doh mazito na machungu lakini sina kuyameza ili nishibe hasa niende kamili kamili asanteni kwakweli nina ninayoyapata kupitia humu ndo maana nikikaa muda napamiss

on November 12, 2015

Kweli mwali wetu, ni bora uyajue mapema hata yakikufika utatambua kuwa wewe si wa kwanza na wala hutakuwa wa mwisho, mwendo ni kupambana tu. Jitahidi uwe juu ya 8020 rule, ufikie 95% badala ya 80% umtie ugumu wa kwenda kuitafuta hiyo 5% nje.

on November 13, 2015

Duh hiyo 95% unaweza ukahisi umefika kumbe mwenzio ndio anaona ndio 50% uwiii ndoa ndoana. Ila cha muhimu usikae na kitu moyoni mwambie mtu wako wa karibu na ww mwenye akili timamu,busara, hekima. kwani kutoa kitu moyoni pia huleta nafuu ila usitangaze kwa  kila mtu

Show more replies
 • Liked by
Reply
Cancel
0 on November 13, 2015

i hope hii maana imesaidia wengi ambao na victims aiseee…kama haupo ndani ya ndoa..unajua tu maana ya harusi kama sherehe..ila ukiingia ndoani…utaona harusi ilikua kama fumbo flan ambalo hujui japo unafuraha….

 • Liked by
Reply
Cancel
0 on November 17, 2015

ila wanawake sisi tuna roho ngumu hivi unajiskiaje kutembea na mume wa mtu mpaka anasahau family yake watoto wanateseka we upo tu unakula raha hata hujistukii??

 • Liked by
Reply
Cancel
Loading more replies